Thursday, October 9, 2014

CRİSTİAN RONALDO KUMALİZİA SOKA LAKE MADRİD

Cristiano Ronaldo hana nia ya kurejea
Manchester United na atamalizia
kucheza soka yake Real Madrid,
amedai wakala wake Jorge Mandes.
Ronaldo, 29, tayari amefunga magoli
15 msimu huu, ikiwemo kufikisha hat
trick 22 katika La Liga. Taarifa
zimekuwa zikimhusisha Ronaldo
kurejea Old Trafford kwa uhamisho
wa pauni milioni 80. Mendes
amesema: "Cristiano ameridhika sana
Real Madrid. Ataendelea kuvunja
rekodi zote hapo na kustaafu hapo."
Wakala huyo amekiambia kituo cha
radio cha Cadena COPE kuwa:
"Huwezi kupata mchezaji mwingine
kama yeye.
"Anaendelea kuwa mchezaji bora, na
ataendelea kuwa hivyo hadi
atakapofika umri wa miaka 40.
"Anaipenda United kwa sababu moyo
wake ulikuwa pale kwa miaka sita.
Lakini sasa vyote anavyofikiria ni Real
Madrid na atakuwepo hapo.
"Ndoto ya Cristiano ni kushinda
Champions League. Huwa bado ana
njaa, na siku zote anataka zaidi.
"Haishi kushangaza watu. Ni vigumu
kupata mtu yeyote kama yeye katika
historia ya soka."
Ronaldo aliondoka Manchester United
kwenda Real Madrid mwaka 2009 kwa
uhamisho wa pauni milioni 80.
Meneja wa Manchester United Louis
van Gaal alikiri mwezi uliopita kuwa
angependa kumsajili kiungo huyo,
lakini hatarajii kama Real Madrid
watakuwa tayari kumuuza.l
      source..supersport

No comments:

Post a Comment